• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Kuelimisha vijana tukipinga miradi ya kuwapa ajira ni kazi bure – Ruto

Kuelimisha vijana tukipinga miradi ya kuwapa ajira ni kazi bure – Ruto

NA PCS

RAIS William Ruto amesisitiza haja ya nguzo tatu za serikali kufanya kazi kwa nia nzuri ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana nchini, hii ikiwa njia mojawapo ya kubuni nafasi za ajira kwa vijana.

Akihutubu wakati wa kuzindua miradi kadhaa katika Kaunti ya Meru, kiongozi wa nchi alisema ofisi ya Rais, Idara ya Mahakama, na Bunge, hufaa kufanya kazi kwa moyo wa kutumikia raia.

Rais Ruto alisikitika huenda tatizo la ukosefu wa ajira likageuka bomu na kulipuka.

Alisema serikali bila kuungwa mkono kikamilifu na mahakama na bunge, haiwezi ikafaulu katika mipango yake ya kuimarisha maisha ya Wakenya.

Baadhi tu ya mipango ya serikali ya Kenya Kwanza kubuni nafasi za ajira ni ule mradi wa ujenzi wa nyumba nafuu, kazi za kidijitali, na kupeleka Wakenya ng’ambo kwa kazi.

“Hatuwezi tukanyamazia suala hili. Ukosefu wa ajira ni changamoto kuu nchini,” akasema Rais Ruto.

Rais alikuwa katika maeneo ya Imenti Kusini, Imenti ya Kati, na and Imenti Kaskazini.

Alisema suala hilo lisiporekebishwa, kuelimisha vijana kwa mabilioni kutakuwa ni kazi bure kama kujaza maji kwa ndoo iliyotoboka.

“Hatuwezi kutumia Sh650 bilioni kila mwaka kuelimisha watoto wetu huku tukiwa bila mipango yoyote ya ubunaji wa nafasi za kazi na fursa nyinginezo,” akasema.

Naye Naibu Rais Rigathi Gachagua aliwataka Wakenya kumuunga mkono Rais Ruto akisema mikakati yake inasaidia Kenya kujinasua kwa mtego wa deni kubwa.

Wengine waliokuwa wameandamana na Rais Ruto kwenye ziara hiyo katika Kaunti ya Meru ni mawaziri Alice Wahome, Moses Kuria, Eliud Owalo, Ezekiel Machogu, na Mithika Linturi, Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah.

Wengine walikuwa ni Seneta wa Meru Kathuri Murungi, wabunge Elizabeth Karambu (Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Meru), Mpuru Aburi (Tigania Mashariki), John Paul Mwirigi (Igembe Kusini), Rindikiri Mugambi (Buuri), John Mutunga (Tigania Magharibi), Shadrack Mwiti (Imenti Kusini), Moses Kirima (Imenti ya Kati) na mbunge maalum Dorothy Muthoni miongoni mwa viongozi wengine.

  • Tags

You can share this post!

Watoto wa Mr Ibu waiba Sh9.9m za kugharimia matibabu yake

DCI yaahidi kuvunja mitandao ya wizi wa magari

T L