• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM
Majonzi nyota wa rekodi ya dunia ya marathon, Kiptum akiaga dunia

Majonzi nyota wa rekodi ya dunia ya marathon, Kiptum akiaga dunia

CAROLINE WAFULA NA BERNARD ROTICH

MSHIKILIZI wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum na kocha wake raia wa Rwanda Garvais Hakizimana wameaga dunia katika eneo la Kaptagat, Elgeyo Marakwet, kupitia ajali mbaya ya barabarani.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili usiku, kulingana na Kamanda wa Polisi wa Marakwet Peter Mulinge.

Kiptum alikuwa anaendesha gari aina ya Toyota Premio, akiwa na abiria wawili – Garvais na mwanamke aliyetambuliwa kama Sharon Kosgey, wakielekea Eldoret.

Sharon aliponea kifo akiwa na majeraha mabaya na alikimbizwa katika hospitali ya Racecourse, huku miili ya mwanariadha huyo na kocha wake ikapelekwa mochari ya hospitali hiyo hiyo.

Gari lao liliharibika vibaya na limepelekwa katika kituo cha polisi cha Kaptagat.

“Hii ilikuwa ajali iliyosababishwa na dereva ambapo Kelvin Kiptum, mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon, alikuwa anaendesha gari akiwa na abiria wawili. Kiptum na Hakizimana walifariki papo hapo, huku mtu wa tatu amekimbizwa hospitali ya Racecourse, Eldoret,” akasema Kamanda huyo wa Kaunti.

Kiptum, ambaye rekodi yake ya marathon ya saa mbili na sekunde 35 ilirasimishwa wiki jana na Shirika la Riadha Duniani, alikuwa anajiweka pazuri kukimbia chini ya saa mbili katika Rotterdam Marathon Aprili 14 mwaka huu.

Alikuwa pia kwenye kikosi cha Kenya kilichochaguliwa kwa michezo ya Olimpiki ya 2024 jijini Paris, Ufaransa kuanzia Julai.

Kulingana na Mulinge, Kiptum alipoteza mwelekeo wa gari na kugonga mti kabla ya kutupwa hadi kwenye mtaro karibu umbali wa mita 60.

  • Tags

You can share this post!

Sababu za kuamua kuchomwa badala ya kuzikwa mwigizaji Ouda...

Jinsi wahamiaji kutoka mashambani wachangia mzigo wa basari...

T L