Habari za Kitaifa

Marais na wageni kutoka nje waliohudhuria ibada ya Raila, Nyayo

Na CHARLES WASONGA October 17th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MARAIS Hassan Sheikh Mohamud (Somalia), Taye Selassie wa Ethiopia  makamu wa rais wa Tanzania Philip Mpango na mwenzake wa Sudan Kusini Rebecca Nyendeng ni miongoni mwa viongozi wengi wa kigeni waliohudhuria ibada ya Kitaifa ya kumuaga Raila Odinga katika uwanja wa Nyayo, Nairobi, Oktoba 17, 2025.

Wengine waliohudhuria ibada hiyo ni aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Waziri wa Masuala ya Ndani nchini Rwanda Vincent Biruta aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

Vile vile, Naibu Rais Kithure Kindiki alitangaza kuwa serikali ilipokea rambirambi kutoka kwa viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika  na ulimwengu.

Miongoni mwa marais waliotuma risala zao ni; Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), John Mahama (Ghana), Hakainde Hichilema (Zambia).

Wengine ni pamoja na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mngagwa, Adama Baro (Gambia), Evariste Ndayishimiye (Burundi), Bola Tinubu (Nigeria), Felix Tshisekedi (DRC), miongoni mwa wengine.

Viongozi wa ulimwengu waliotuma risala zao ni pamoja na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutterres na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (WHO) Tedros Adhanon Ghebreyesus.