• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Mjeledi wa Waziri Kindiki kwa polisi wanaocheza karata na sheria za pombe

Mjeledi wa Waziri Kindiki kwa polisi wanaocheza karata na sheria za pombe

NA TITUS OMINDE

WAZIRI wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki amewataka maafisa wa polisi na watumishi wengine wa umma kuchagua kati ya kuuza pombe na kuacha kazi. 

Akihutubu Mjini Kitale mnamo Jumatatu, Machi 18, 2024 Prof Kindiki alisema maafisa wa polisi pamoja nawafanyikazi wa KRA, ACA, KEBS miongoni mwa mashirika mengine ya serikali ambayo huhusika na kampeini ya kukabiliana na pombe haramu wenye baa, sharti wafunge baa zao la sivyo wajiuzulu kazini.

Kushiriki kwenye biashara ya pombe, Bw Kindiki alisema maafisa hao huhitilafiana na kampeni dhidi ya pombe haramu na hatari hivyo basi wanapswa kujiuzulu au wazikomeshe.

Naibu Rais, Rigathi Gachagua anaongoza oparesheni dhidi ya pombe haramu, hatari na dawa za kulevya ambapo ameapa kukabiliana na wahusika.

“Ikiwa wewe ni polisi, afisa wa KRA, KEBS, ACA miongoni mwa mashirika mengine ya serikali na unafanya biashara ya pombe ni lazima ujiuzulu la sivyo ufunge baa yako,” alisema Bw Kindiki.

Waziri alifichua kuwa zaidi ya maafisa 40, 000 wa polisi watahamishwa, hatua hiyo ikilenga waliokaa kwenye stesheni wanazohudumu kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Maafisa wote wa polisi ambao wamehudumu katika kituo kimoja cha polisi kwa zaidi ya miaka mitatu, lazima wahamishwe katika muda wa mwezi mmoja ujao. Mpango huo unaendelea. Tayari tumehamisha zaidi ya maafisa 10, 000 na tunalenga kuhamisha jumla ya maafisa 42,500 haraka iwezekanavyo,” akasisitiza Bw Kindiki.

Aidha, alitoa makataa ya muda usiojulikana kwa maafisa wa polisi na maafisa wengine wa serikali wanaoendesha biashara ya pombe kufunga baa zao.

“Kupitia baraza la usalama la kitaifa, tumeagiza maafisa wote wa umma wanaojihusisha na biashara yoyote inayohusiana na pombe kwamba lazima waache au wajiuzulu mara moja,” alisema Bw Kindiki.

Waziri huyo alisema maafisa wanaohusika na biashara ya pombe wana mgongano wa kimaslahi, hivyo basi kulemaza juhudi za serikali kukabiliana na pombe haramu.

Aliwataka viongozi wa kisiasa kutoingilia mpango huo ili kufanikisha azma ya serikali kukabiliana na pombe haramu.

“Viongozi wote wa kisiasa wakae mbali. Wajue kwamba hili si suala la kisiasa, bali ni utekelezaji sheria.”

Alisema Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi, IG Japhet Koome na wadauhusika wengine wakuu katika idara ya usalama wamejitolea kukabiliana na kero ya pombe haramu na hatari.

  • Tags

You can share this post!

‘Wana’ wa Ruto wakabana koo kuhusu madai ya hongo ya...

Shule za upili kusubiri siku 10 kupata ufadhili wa serikali...

T L