Habari za Kitaifa
Mshukiwa wa mauaji Kware adai kuteswa ndio akiri kuua wanawake 42

Mshukiwa wa mauaji Kware, Collins Jomaisu Khalisia alipokamatwa na polisi Jumatatu. Picha|Maktaba
MSHUKIWA wa mauaji ya kutatanisha ambayo miili ilipatikana kwenye magunia katika timbo la kina kirefu eneo la Kware, Embakasi ameambia hakimu kwamba alipigwa ili akubali kutenda makosa hayo.
Collins Jumaisu Khalisia aliambia hakimu Irene Gichobi wa Mahakama ya Makadara Jumanne, Julai 16, 2024 kwamba alipigwa na maafisa wa polisi ili akiri kuhusika katika mauaji ambayo yameshtua nchi.
Hakimu amekubalia polisi kumzuilia kwa siku 30 kabla ya maagizo zaidi kutolewa.