• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Muturi aonya KRA kuhusu ushuru wa nyumba

Muturi aonya KRA kuhusu ushuru wa nyumba

NA BONFACE OTIENO

MWANASHERIA Mkuu Justin Muturi ameionya Mamlaka ya Ushuru nchini (KRA) dhidi ya kuendelea kukusanya ushuru wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu ambao ulitangazwa kuwa haramu na Mahakama ya Rufaa mnamo Januari 26, 2024.

Kamishna Mkuu wa KRA Humprey Wattanga katika barua yake Februari 12,2024 aliomba mwongozo kutoka kwa AG kuhusu msimamo wa serikali kuhusu ushuru huo.

Bw Muturi alisema ushuru huo ulikosa msingi wa kisheria wakati wa uamuzi wa Mahakama hivyo KRA haifa kuendelea kukusanya ushuru huo.

“Ilibainika kwamba, ushuru huo hauna msingi kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 84 cha Sheria ya Fedha,” Muturi alisema katika barua ya Februari 21,2024 kwa Bw Wattanga.

“Kwa hiyo, rai yetu ni kwamba, hadi tarehe ya kutolewa kwa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa yaani Januari 26, 2024, hakuna kifungu cha kisheria kinachotoa idhini ushuru huo kuendelea kukusanywa,” aliongeza katika barua hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Shahidi katika kesi ya mauaji adai Jumwa alimlima makonde

Watalii wang’ang’ania mfupa wa nyangumi kupiga...

T L