• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:52 PM
Ni njia tofauti za upendo au mgawanyiko?

Ni njia tofauti za upendo au mgawanyiko?

NA CHARLES WASONGA

JAMBO la kushangaza limetokea katika familia ya marehemu Mhandisi Kata Matemu Kithyo aliyefariki Aprili 18, 2024 mjini Mombasa baada ya wake zake wawili kuwake matangazo mawili tofauti kuhusu kifo chake siku moja na katika gazeti moja.

Matangazo hayo mawili yaliyochapishwa katika gazeti la ‘Daily Nation’ toleo la Aprili 23, 2024, yanatoa taswira ya nyumba mbili katika familia ya marehemu kuamua kufanya vitu viwili tofauti.

Je, ni njia tofauti za upendo au ni mgawanyiko?

Uchunguzi wetu umebaini kuwa wake wa marehemu Kithyo–Prisca Mukethe Kithya na Agnes Murorunkwere Kata– ndio waliogharamia matangazo hayo tofauti japo yenye lengo la kutangaza kifo chake. Moja liliwekwa kwenye ukurasa wa 37 na jingine katika ukurasa wa 39 wa gazeti hilo hilo la ‘Daily Nation‘.

Katika tangazo la tanzia lililochapishwa katika ukurasa wa 37, Prisca anajitambulisha peke yake kuwa ni mke wa marehemu.

Aidha, imeorodhesha majina ya watoto wake kuwa ni Mark Muinde Kithyo, Melany Mwelu Kithyo na Ruth Kivinyo Kithyo.

Pia imeorodhesha majina ya kaka zake marehemu akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Mumo Matemo.

Tangazo hilo linasema kuwa maelezo zaidi kuhusu mipango ya mazishi itatuliwa baadaye. Na wenye maswali wanaweza kumuuliza Mark Muinde kupitia nambari yake ya simu.

Katika picha iliyotumika katika tangazo hilo inaonekana kama ya zamani kwani marehemu Kithyo anaonekana mwenye umri mdogo kiasi huku akivalia kofia ya kawaida.

Tangazo la pili linamtambua Grace Murorunkwere Kata kuwa ni mke wa marehemu Mhandisi Kithyo na watoto wake.

Picha iliyotumika inaonekana kama ya hivi karibuni, na marehemu amevalia kofia aina ya ‘cowboy’.

Aidha, tangazo limetoa maelezo kwamba jamaa na marafiki wanakutana katika Kanisa la Methodist, kando ya barabara ya Ngong, Nairobi kupanga mazishi kuanzia Aprili 23, 2024 hadi Aprili 26, 2024 kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni. Siku hizo ni Jumanne wiki hii hadi Ijumaa wiki hii.

Shughuli ya kuchanga pesa za kugharimia maandalizi ya mazishi pia ilifanyika katika ukumbi mmoja wa Kanisa lilo hilo, mnamo Jumatano.

Tangazo hilo pia linamtambua marehemu kuwa kakake Bw Matemo miongoni mwa wengine.

  • Tags

You can share this post!

UDA: Ruto awatoa mnofu mdomoni maafisa walafi wa pesa za...

Letoo akiri ‘kuangusha’ wageni kwa kuweka hema...

T L