Papa Francis alazwa hospitali kwa uchunguzi na matibabu
KIONGOZI wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis Ijumaa asubuhi alipelekwa hospitalini kwa vipimo na matibabu yanayoendelea ya mkamba, makao makuu ya kanisa hilo Vatican yalisema.
Hili ni tukio la hivi punde zaidi la papa huyo mwenye umri wa miaka 88 kupata tatizo la kiafya.
“Leo asubuhi, baada ya hotuba yake, Papa Francis alilazwa katika hospitali ya Policlinico Agostino Gemelli kwa vipimo muhimu vya uchunguzi na kuendelea na matibabu yake ya mkamba, ambayo amekuwa akipata katika mazingira ya hospitali,”Vatican ilisema katika taarifa.
Papa Francis aliyechaguliwa papa 2013 ameugua mafua na matatizo mengine ya kiafya mara kadhaa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Mapema mwezi huu, Francis aliwaambia mahujaji kwamba alikuwa akisumbuliwa na “baridi kali,” ambayo Vatican baadaye ilitaja kama ugonjwa wa mkamba.
Papa amekuwa akizingatia ratiba yake ya kila siku licha ya ugonjwa wake, akifanya mikutano katika makazi ya Vatican anakoishi. Kabla ya kwenda hospitalini Ijumaa, alikuwa na mkutano rasmi na Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico.
Francis pia alifanya mikutano Ijumaa asubuhi na Kadinali Luis Tagle, afisa mkuu wa Vatican, na kikundi cha wahisani cha Kikatoliki kilichoko Puerto Rico na Mark Thompson, mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha habari cha CNN.
Mmoja wa watu waliohudhuria moja ya mikutano hiyo, ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alisema Papa alionekana kutatizika kuzungumza wakati wa mkutano kwao.
Francis alianguka mara mbili hivi majuzi katika makazi yake ya Vatican, akachubuka kidevu Desemba na kuumia mkono Januari.
Hospitali ya Gemelli ndiyo kubwa zaidi jijini Roma, na ina chumba maalum cha kuwatibu mapapa. Mnamo Juni 2023, Papa Francis alikaa huko kwa siku tisa akifanyiwa upasuaji