Habari za Kitaifa

Pasta Ezekiel alivyomtetemesha mwenzake Benny Hinn kwa kutoa Sh14.6m

February 28th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA WANDERI KAMAU

PASTA Ezekiel Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre, Kilifi, alitoa mchango wa Sh14.6 milioni wakati mkutano wa maombi wa Pasta Benny Hinn kutoka Amerika, uliofanyika Jumatatu katika Uwanja wa Michezo wa Nyayo, jijini Nairobi.

Hinn, aliyeongoza mkutano huo kati ya Jumamosi na Jumapili katika uwanja huo, alianza kuchangisha pesa hizo kuwasaidia waandalizi wa maombi hayo kulipia gharama ya maandalizi yake.

Waandalizi walikuwa na deni la Sh14.6 milioni.

Mhubiri huyo alisema ijapokuwa haikutarajiwa kwamba angelipa deni hilo, “angesikitika kuwaacha waandalizi hao na deni hilo”.

Pasta Ezekiel alitoa mchango huo baada ya Pasta Hinn kuwaalika wahisani kujitokeza kuwasaidia waandalizi kumalizia deni hilo.

Pasta mmoja kutoka China ndiye alikuwa wa kwanza kwa kutoa mchango wa Sh2 milioni.

Wakati mkutano huo ulikuwa ukiendelea, Pasta Ezekiel alimtuma mwakilishi wake kwenye jukwaa kuu kumwambia Hinn kuwa angetoa Dola 100,000 (ambazo ni Sh14.6 milioni).

“Nina habari njema kwenu, Mtumishi Ezekiel kutoka Kenya; Wakenya mnamjua vyema sana. Amesema kuwa Mtumishi wa Mungu (Hinn) anafaa kuachwa kuendelea kuiombea Kenya kupata upako. Atasimamisha moja ya shughuli zake kesho na atatuma Sh14.6 milioni (Dola 100,000),” akasema mwakilishi huyo.

 Baadhi ya watu maarufu waliohudhuria maombi hayo ni Rais William Ruto, mkewe Rais; Bi Rachel Ruto, Naibu Rais Rigathi Gachagua na mkewe, Bi Dorcas Gachagua