• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Pendekezo moja kuhusu ushuru wa nyumba ambalo Wabunge wametii

Pendekezo moja kuhusu ushuru wa nyumba ambalo Wabunge wametii

NA MWANDISHI WETU

HUENDA waajiri wakapata afueni kubwa ikiwa Bunge la Kitaifa litaidhinisha pendekezo la kamati yake la kuondolewa kwa waajiri kulipa asilimia 1.5 kama ushuru wa nyumba sawa na waajiri wao.

Sheria ya Fedha wa 2023 iliyopitishwa bungeni Juni 28, 2023 inatoa pendekezo hilo ambalo limepingwa vikali na waajiri (kupitia Shirikisho lao-FKE) wakisema linawaongezea gharama.

Lakini sasa Kamati ya Pamoja ya Bunge la Kitaifa kuhusu Fedha na ile ya Nyumba iliyokusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu Mswada wa Nyumba za Gharama Nafuu limekubaliana na malalamishi ya waajiri kuwa hitaji hilo litachangia watu wengi kufutwa kazi.

“Kwa hivyo tunapendekeza kuwa bunge hili liifanyie marekebisho Mswada wa Nyumba za Gharama Nafuu ili kuwakinga waajiri wasilipe ushuru wa nyumba wa asilimia 1.5 ya mishahara ya waajiri wao kila mwezi. Hatua hii itazuia hali ambayo watalazimika kuwafuta kazi wafanyakazi wengi ili kupunguza gharama,” kamati hii inasema kwenye ripoti yake.

Akianzisha mjadala kuhusu ripoti hiyo, kiongozi wa wengi Kimani Ichung’wah alisema marekebisho hayo yatawakinga waajiri dhidi ya kulipa ushuru huo kama waajiri wao na hivyo kuwapa afueni.

“Ipo haja ya waajiri kupunguziwa mzigo wa gharama kwa wafanyakazi wao kwa kuondolewa ushuru huu wa nyumba. Hii itazuia hali ambapo baadhi yao watalazimika kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi wao,” akaeleza Bw Ichung’wah ambaye pia ni Mbunge wa Kikuyu.

Hata hivyo, ripoti ya kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Molo Kuria Kimani (mwenyekiti wa Kamati ya Fedha) na Johanna Ng’eno (Mwenyekiti wa Kamati ya Nyumba) inashikilia kuwa waajiri waendelee kulipa ushuru huo wa asimilia 1.5 ya mishahara kila mwezi.

Hata hivyo, mnamo Novemba 26, 2023 Mahakama Kuu iliharamisha ushuru huo kwa misingi kuwa inalenga watu wanaopokea mishahara kila mwezi pekee na kuwasaza wale waliojiajiri.

Mnamo Januari 26, mwaka huu, Mahakama ya Rufaa ilikataa kubatilisha uamuzi wa mahakama hali inayoashiria kuwa serikali inakiuka agizo la mahakama kwa kuendelea kutoza ushuru huo.

Mbunge wa Kathiani Robert Mbui alihoji sababu serikali inaendelea kuwatoza wafanyakazi ushuru huo kinyume na maagizo ya mahakama.

“Mahakama imeharamisha ushuru huu, sasa mbona serikali inaidharau na kuendelea kuutoza wafanyakazi? Wale ambao wamekatwa pesa hizo kwa mshahara wao wa Januari wanapasa kurejeshewa pesa hizo,” akasema Bw Mbui ambaye pia ndiye naibu kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa.

  • Tags

You can share this post!

‘Paka Mzee’ Pennant ajinasia mpenzi mpya baada...

Jifunze namna ya kutumia jiwe la kusaga unga kitamaduni

T L