Habari za Kitaifa
Rais Ruto ateua Ethekon kuwa mwenyekiti mpya wa IEBC

Erastus Edung Ethekon ambaye ameteuliwa na Rais William Ruto kuwa mwenyekiti mpya wa IEBC. Picha|Maktaba
RAIS William Ruto amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa mwenyekiti mpya wa IEBC, katika tangazo la hivi punde zaidi.
Rais pia ameamua kwamba Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu, Moses Mukhwana, Mary Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Aduol na Fahima Abdallah wawe makamishna, hatua ambayo itakamilisha kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kwa ajili ya uchaguzi wa 2027.
Hatua inayofuata ni majina hayo kupelekwa Bunge kwa msasa wa mwisho kabla ya kuapishwa.
Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…