• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 6:30 PM
Rais Ruto, Jaji Koome hatimaye wakutana baada ya wiki nyingi za malumbano

Rais Ruto, Jaji Koome hatimaye wakutana baada ya wiki nyingi za malumbano

NA SAM KIPLAGAT

JAJI Mkuu Martha Koome Jumatatu Januari 22, 2024 asubuhi amekutana na Rais William Ruto na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula katika Ikulu ya Nairobi.

Jaji Mkuu akiwa mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) aliomba kufanyika kwa mkutano huo wiki iliyopita, kufuatia wiki kadhaa za malumbano na lawama dhidi ya Mahakama kutokana na tuhuma za ufisadi.

Wengine kwenye mkutano huo ni Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Mkuu wa Sheria Justin Muturi na Mwanasheria wa Serikali Shadrack Mose.

JSC iliitisha mkutano na Rais wiki jana ili kujadili masuala ambayo Rais amekuwa akiibua kuhusiana na madai ya ufisadi katika Mahakama.

“Jaji Mkuu aliitisha mkutano, na nataka kusema kwamba nakubali mazungumzo. Mnamo Januari 2, nilisema kwamba tunahitaji mazungumzo kuhusu jinsi tutakabiliana na ufisadi,” Dkt Ruto alisema Jumanne iliyopita alipokuwa anahutubia wananchi wa Tindiret, Kaunti ya Nandi.

Jaji Koome ameshikilia kwamba ulikuwa msimamo wa Tume ya JSC kwamba ufisadi au utovu wa nidhamu katika Mahakama ushughulikiwe haraka iwezekanavyo.

Alisema kwamba uaminifu katika utendakazi wa mahakama ni jambo lisiloweza kufanyiwa mchezo akisema ni muhimu katika utendaji haki.

Jaji Mkuu pia aliongeza kwamba JSC imeendelea kukabiliana vyema na madai yote ya ufisadi yaliyowasilishwa mbele yake.

  • Tags

You can share this post!

Wanaume wenye matiti makubwa wamo katika hatari ya kufariki...

Hatutabeba mtu yeyote mpaka wenzetu waachiliwe, bodaboda wa...

T L