Habari za Kitaifa

Serikali yapiga marufuku dawa ya kikohozi Benylin kufuatia madai ya maafa Afrika Magharibi

April 11th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA MWANDISHI WETU

BODI ya Dawa na Sumu nchini imesimamisha mara moja uuzaji na utumiaji wa dawa ya kikohozi ya watoto, kwa jina Benyline Paediatric cough syrup (Batch No 329304).

Hii ni kufuatia kile bodi hiyo imesema ni madai ya maafa katika nchi za Afrika Magharibi yaliyoripotiwa kufuatia matumizi ya dawa hiyo maarufu.

Bodi hiyo sasa inashauri Wakenya kuacha kutumia dawa hiyo mara moja na kupiga ripoti kwa kituo cha afya kilicho karibu iwapo yeyote aliyetumia atapatwa na dalili mbovu.

Maelezo zaidi ni kadiri tunavyoyapata…