• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 AM
Tom Mshindi ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya KBC

Tom Mshindi ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya KBC

NA CHARLES WASONGA

RAIS William Ruto amemteua aliyekuwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa shirika la habari la Nation Media Group (NMG) Tom Mshindi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Shirika la Utangazaji Nchini (KBC).

Kupitia tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali toleo la Januari 19, 2024, Rais Ruto alisema uteuzi huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu unaanza kutekelezwa mara moja.

“Miye William Samoei Ruyo namteua Tom Mshindi Nyamancha kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Nchini (KBC) kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Januari 19, 2024,” Rais akasema kupitia tangazo hilo.

Bw Mshindi atachukua nafasi ya Benjamin Maingi aliyeachishwa kazi.

Mwenyekiti huyo mpya, ambaye pia ni mwanahabari mwenye uzoefu mkubwa, alihudumu katika shirika la NMG kuanzia ngazi ya ripota na akapanda ngazi hadi kuwa Mhariri Mkuu Mtendaji.

Bw Mshindi alistaafu mnamo 2018 baada ya kuhudumu katika NMG kwa miaka 24.

Uteuzi wa Mshindi unajiri mwezi mmoja baada ya KBC kumfuta kazi Mkurugenzi Mkuu Samuel Maina kuhusiana na sakata ya kandarasi fulani tata.

Bw Maina alipigwa kalamu na Waziri wa ICT Eliud Owalo kwa kulipa Sh750 bilioni kwa shirika moja la kutatua mizozo bila idhini kutoka wizara hiyo.

Baadaye waziri huyo alimteua mtaalamu katika masuala ya uchumi Paul Macharia kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa KBC.

  • Tags

You can share this post!

Obama amwaga jumbe za kumsifia mkewe

Utakachokatwa kwenye mshahara kwa ajili ya bima mpya ya...

T L