TSC: Tunahitaji walimu 20,000 zaidi kujaza pengo JSS
NA WANDERI KAMAU
TUME ya Kuwaajiri Walimu Nchini (TSC) imesema inahitaji fedha kuajiri karibu walimu 20,000 wa Sekondari Msingi (JSS) kote nchini.
Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo, Bi Nancy Macharia, alisema kuwa tume hiyo inahitaji jumla ya walimu 96,000 kuendesha mfumo wa Elimu ya Umilisi na Utendaji (CBC), ijapokuwa ni walimu 53,000 waliopo kwa sasa.
“Ingawa tuna hatua zilizochukuliwa kulainisha mfumo huu wa elimu, bado tuna uhaba mkubwa wa walimu unotukabili. Wito wetu kwa serikali ni kutuongeza mgao wa fedha ili kujaza pengo hilo,” akasema Bi Macharia.
Kwa sasa, walimu wanaofunza katika JSS wameajiriwa kwa mfumo wa kandarasi.
Tayari, baadhi yao wametishia kugoma ikiwa hawataajiriwa kwa mfumo wa kudumu.