• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Wakana ulaghai wa zaidi ya Sh1 milioni

Wakana ulaghai wa zaidi ya Sh1 milioni

NA RICHARD MUNGUTI
WASHUKIWA watatu wamefikishwa kortini kwa ulaghai wa Sh1.1 milioni.

Farrah Osman Issak, Abdiakin Ismail Abdullahi na Godfrey Otieno Omwoyo almaarufu Kassim, walishtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Mahakama ya Milimani, Lucas Onyina.

Wakati wa kumlaghai Bw Ahmed Ali Mohammed katika eneo la Eastleigh, Kaunti Ndogo ya Kamukunji, washtakiwa hao walidai walikuwa na uwezo wa kumletea simu za rununu kutoka ng’ambo.

Walishtakiwa kwa kupokea pesa hizo kati ya Machi 2 na 16 2024.
Bw Onyina alielezwa na kiongozi wa mashtaka Bi Mercy Kwamboka kwamba  washtakiwa walijifanya walikuwa na uwezo wa kumwagizia kutoka ng’ambo simu za kiunga mbali.

Issak na Abdulahi walikabiliwa na shtaka mbadala la kupatikana na pesa bandia.

Aidha, walikana walikutwa na Dola za Amerika bandia.

Mahakama iliambiwa kuwa walipatikana wakiwa na pesa hizo ndani ya lojing’i katika eneo la Kamkunji walipotiwa nguvuni mnamo Machi 16,2024 na maafisa wa upelelezi (DCI) kutoka eneo la kati mwa Nairobi.

Makachero wa Idara ya Ujasusi (NIS) ndio waliowapasha maafisa wa DCI habari hizo za ulaghai na ufisadi.

Baada ya kukana mashtaka washtakiwa waliomba waachiliwe kwa dhamana.

Bi Kwambo hakupinga ombi hilo na kila mmoja aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000 ama dhamana mbadala ya Sh300, 000 pesa tasilimu.

Mahakama ilielezwa kwamba polisi watawasilisha mashtaka ya ziada dhidi ya washtakiwa hao ya kupatikana na pesa bandia.

  • Tags

You can share this post!

DJ Joe Mfalme kuzuiliwa siku 14 katika kesi ya mauaji ya...

Afisa katika kesi ya ulaghai wa shamba la mabilioni...

T L