• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Walimu wasio na kazi wasubiri TSC itangaze nafasi 20,000

Walimu wasio na kazi wasubiri TSC itangaze nafasi 20,000

NA WANDERI KAMAU

Hayo yalielezwa Alhamisi na Kamati ya Bajeti na Matumizi ya Bunge, inayoongozwa na mbunge Ndindi Nyoro (Kiharu), kwenye Taarifa ya Kutayarisha Bajeti.

Taarifa hiyo ndiyo huwa inatolewa kwanza kabla ya bajeti yenyewe kusomwa.

Taarifa hiyo huwa inaeleza mipango na mikakati ambayo Serikali ya Kitaifa na zile za kaunti zimeweka kwenye matayarisho ya bajeti zao.

Kamati hiyo pia ilipendekeza Idara ya Kusimamia Elimu ya Juu kutengewa Sh131 bilioni, huku elimu ya vyuo vikuu ikitengewa Sh130.2 bilioni.

Taasisi za Mafunzo ya Kiufundi zilitengewa jumla ya Sh30.4 bilioni.

Mwaka 2023, Rais William Ruto alisema kuwa serikali itaitengea fedha zaidi TSC, ili kuiwezesha kupunguza pengo lililopo baina ya walimu na wanafuzi.

Kufikia sasa, serikali imewaajiri walimu 56,000 ingawa imekuwa ikihimizwa kuwaajiri kwa mfumo wa kudumu, kwani wengi wao wameajiriwa kwa njia ya kandarasi.

Tangazo linajiri siku chache baada ya ripoti moja kufichua kwamba ni asilimia 60 pekee ya walimu nchini walioajiriwa na TSC, huku asilimia 40 wakiajiriwa na wazazi au Bodi za Kusimamia Shule (BOMs).

Ripoti hiyo, ambayo ilitolewa na shirika la Usawa Agenda, ilionyesha kuwa asilimia tisa ya walimu ni wanafunzi-walimu walio katika masomo ya nyanjani.

Zaidi ya hayo, ilifichua kwamba asilimia sita ya walimu walio katika shule za serikali za msingi hawana mafunzo rasmi ya ualimu.

Idadi kubwa ya walimu hao wamekuwa wakihudumu kwenye vituo ambako serikali haijawatuma walimu.

Kulingana na ripoti hiyo, shule za msingi zilizo katika maeneo ya mashambani ndizo zimekuwa zikiathiriwa sana na ukosefu wa walimu wa kutosha.

Ripoti ilieleza masaibu ambayo walimu wengi walioajiriwa na wazazi huwa wanapitia, kwani asilimia 20 huwa wanalipwa mishahara ya kati ya Sh10,000 na Sh20,000.

Ilieleza kuwa ni asilimia moja pekee ya walimu hao ambao huwa wanalipwa kati ya Sh20,000 na Sh30,000.

  • Tags

You can share this post!

Kinaya nduguye Monicah kumtaka Jowie kupasha wanahabari...

Ruto amteua dadake Raila kuwa naibu mkuu wa ubalozi mdogo

T L