• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Wizara ya Kilimo kutuma wakaguzi kutekeleza kanuni za miraa

Wizara ya Kilimo kutuma wakaguzi kutekeleza kanuni za miraa

NA DAVID MUCHUI

WIZARA ya Kilimo itatuma wakaguzi wa usalama wa chakula katika Kaunti ya Meru ili kutekeleza kanuni za miraa eneo hilo.

Kanuni za Miraa 2023, zinalenga kulinda usalama wa chakula na viwango vya ubora wa miraa pamoja na kukuza mbinu bora katika uzalishaji, usindikaji, uuzaji, ukusanyaji na usafirishaji wa zao hilo.

Kanuni hizo pia zilianzisha ulipaji wa ushuru wa Sh3 kwa kilo moja ya miraa inayouzwa soko la ng’ambo.

Waziri wa Kilimo, Mithika Linturi Jumapili, Aprili 7, 2024 alisema wizara yake ilikuwa ikifanya kazi usiku na mchana kutekeleza kanuni hizo akibainisha kuwa ‘mustakabali wa miraa unalenga kuongeza thamani’.

“Kama sehemu ya juhudi za kutekeleza kanuni za miraa, tunakamilisha ujenzi wa jumba la kupakia miraa katika soko la Muringene, Igembe ya Kati. Wakulima na wafanyabiashara watahitajika kuzingatia viwango vya kimataifa vya usafi wa chakula katika kushughulikia miraa. Hivi karibuni tutatuma maafisa wa kutekeleza sheria ili kuhakikisha hili linafuatwa hadi viwango hivyo vikumbatiwe,” Bw Linturi alisema.

Kanuni hizo zinaitaka Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) kusajili na kutoa leseni kwa wanaofanya kazi katika vitalu vya miraa, vyama vya wakulima, maajenti, wasafirishaji wa miraa, wachuuzi, waagizaji na wauzaji miraa nje ya Kenya.

Waziri Linturi alisema kutekelezwa kwa kanuni hizo kutasaidia serikali kupata masoko zaidi ya zao hilo huku kukiwa na wasiwasi wa kupungua kwa mahitaji na kushuka kwa bei ya zao hilo.

 

  • Tags

You can share this post!

Mgawanyiko chama cha Ruto, UDA

Chifu na mwanawe taabani kwa tuhuma za mauaji ya mfanyakazi

T L