Habari

Hofu kuhusu idadi kubwa ya wanafunzi wanaokamilisha elimu ya msingi kabla wajue kusoma na kuandika

September 20th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MAGDALENE WANJA

BENKI ya Dunia imeelezea hofu kuhusu idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi ambao wanakamilisha elimu ya msingi kabla wajue kusoma na kuandika.

“Kama watoto hawatajua kusoma,hawataweza kujiendeleza na kukua kama binadamu anavyotakiwa,” akasema mkuu wa mpango wa walimu wa SABER chini ya Kitengo cha Maarifa ya Kimataifa na Ubunifu, Ezequiel Molina.

Monila hata hivyo amesifu mpango wa Tusome kwa kusaidia katika kudumisha elimu ya msingi.

Monila alizungumza baada ya kutembelea wanafunzi katika darasa moja katika shule ya Umoja I Primary School wakati wa somo la Kiswahili.

Anaongoza kikundi cha watafiti wanaozuru nchi za Bangladesh, Nigeria, Ethiopia, Nepal, Tanzania, Sudan, Senegal, na Msumbiji.

Afisa katika Wizara ya Elimu Bi Hellen Boruett ameongoza kikundi hicho cha watafiti.

Mpango huo wa Tusome chini ya shirika la USAID unagharimu Dola za Kimarekani 53.8 milioni.