Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga kuanza huduma za rufaa Januari
HOSPITALI ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH) Kaunti ya Kisumu inatarajiwa kuanza kutoa huduma za hospitali ya rufaa ya kitaifa mwishoni mwa Januari.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt Joshua Clinton Okise, alisema Alhamisi, Desemba 18, 2025 kwamba kamati ya mpito ilikamilisha jukumu lake mnamo Desemba 11 na kukabidhi rasmi ripoti yake kwa bodi ya usimamizi wa hospitali, Idara ya kaunti ya Huduma za Matibabu na afisi yake.
Akizungumza na vyombo vya habari katika hospitali hiyo mjini Kisumu baada ya mkutano wa wafanyakazi, Dkt Okise alisema mchakato huo umezingatia nguzo tatu muhimu – rasilimali, sheria, na uhamishaji wa mali na fedha.
ili kuleta utulivu katika hospitali hiyo kufuatia kupandishwa hadhi kwake hadi ya rufaa ya kitaifa.’Mfumo wa usimamizi wa mishahara tayari umehamishwa kikamilifu kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Kisumu hadi JOOTRH. Sasa tunalipa wafanyikazi wetu moja kwa moja, na tangu mabadiliko hayo, mishahara imekuwa ikilipwa tarehe 27 kila mwezi,’ alisema.