Habari

Jaji aamuru NTSA iachilie matatu zikiwemo za mwanawe Rais Ruto

Na RICHARD MUNGUTI February 3rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MAHAKAMA Kuu imeiamuru Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi Barabarani (NTSA) iachilie matatu zote ilizokamata wakati wa msako wa magari mabovu ikiwemo ya George Ruto, mwanawe Rais William Ruto.

Na wakati huo huo, Jaji Bahati Mwamuye aliamuru nambari za usajili za matatu hizo zilizong’olewa na maafisa wa NTSA na polisi zirudishiwe wamiliki mara moja.

Jaji Mwamuye alitoa agizo hilo kufuatia kesi iliyowasilishwa na wakili Danstan Omari aliyemweleza kuwa wahudumu hao wa matatu wamepata hasara isiyopungua Sh5 bilioni.

Wahudumu wa chama cha MCA Sacco kinachomiliki matatu zilizopambwa kwa picha za kupendeza na kucheza muziki walieleza Jaji Mwamuye kwamba hakuna sheria inayoruhusu polisi au NTSA kung’oa nambari za usajili.