Jinsi Orengo, Sifuna walikaa ngumu mbele ya Ruto
GAVANA wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna Jumamosi waliendeleza upinzani wao kwa serikali jumuishi wakiikosoa mbele ya Rais William Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga.
Bw Orengo na Bw Sifuna wamekuwa wakionyesha upinzani kwa ushirikiano kati ya Rais na Bw Odinga wakati viongozi wengine wa ODM wakisifu hatua hiyo na kusema itasaidia maeneo ya upinzani kunufaika na miradi ya maendeleo.
Walikuwa wakiongea wakati wa mazishi ya mlinzi wa kibinfasi wa Raila, marehemu George Oduor katika, eneobunge la Rarieda, Siaya.
“Mkiendelea kuwa kibaraka hatutakuwa na nchi,” akasema Bw Orengo.
Kwa upande wake, Bw Sifuna alimkumbusha Rais Ruto kuhusu mkataba ambao ODM ulitia saini na UDA na pia akamtaka Rais awafute kazi baadhi ya wanaopaka tope serikali yake.