Habari

Kalameni atoroka kazini baada ya kumfunga binti wa mdosi bao la mahaba

Na DENNIS SINYO December 10th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MILIMANI, KITALE

POLO aliyekuwa akifanya kazi hapa alitoroka baada ya binti ya mdosi wake kudai alikuwa na ujauzito wake.

Duru zadai mwanadada huyo alimnyemelea jamaa huyo muda mfupi tu baada ya kuajiriwa na babake.

Licha ya mzee kuwa mkali, kipusa huyo aliamua kwenda kinyume na masharti ya babake na akamuingiza boksi polo huyo.

Hivi majuzi, demu alimweleza jamaa alikuwa na ujauzito na kumtaka ajiandae kuwajibika babake akizusha.

“Nina ujauzito wako na lazima ujipange jinsi tutalea huyu mtoto kwa sababu babangu hatakubali nikae hapa,” alimwambia jamaa.

Siku iliyofuatia, polo alibeba nguo zake na kuhepa akidai hakuwa tayari kuoa.