Habari
Kalonzo ndiye ataupeleka upinzani Bondo
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka. Picha|Hisani
VIONGOZI wa upinzani watavamia Bondo kwa kishindo Alhamisi hii kumwomboleza na kumuenzi aliyekuwa waziri mkuu marehemu Raila Odinga.
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka alitangaza kuwa watafika Kangó ka Jaramogi ambako Raila alizikwa na nyumbani kwake Opoda kumwomboleza.
Alizungumza kwenye hafla moja na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye bado haijafahamika iwapo atakuwa kwenye ziara hiyo.