Habari

Majonzi watoto watatu wakiaga kwenye choo kibovu shuleni mwao Uasin Gishu

Na BARNABAS BII July 10th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

WANAFUNZI watatu Alhamisi, Julai 10, 2025 walifaruju na wengine kupata majeraha baada ya choo kuanguka katika Shule ya Msingi ya Queen of Angels, Kaptebee, Kaunti ya Uasin Gishu.

Ilibainika wanafunzi hao walikwama wakati ukuta wa choo cha shule hiyo kiliporomoka kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha eneo hilo.

Afisa wa upelelezi wa jinai akirekodi matukio katika shule ya Queen of Angels Mission School mjini Turbo baada ya watoto watatu kufariki kwa kuporomokewa na choo. Picha|Jared Nyataya

Kamishina wa Polisi wa Uasin Gishu Dkt Edison Nyale alisema kuwa walikuwa wakitumia choo hicho wakati kiliporomoka.

Sakafu ya choo hicho iliporomoka na watoto hao wakakwama ndani,” akasema Dkt Nyale.

Watoto wanne waliondolewa ndani ya choo hicho huku watatu wakifa wakipelekwa katika Hospitali ya Kaunti ndogo ya Turbo.

Juhudi za uokoaji zilizoshirikisha maafisa kutoka Huduma ya Kitaifa kwa Vijana (NYS), wasamaria wema na idara ya zimamoto kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, zilikuwa zikiendelea.

Watoto walionusurika walipelekwa hadi Hospitali ya Kaunti ya Turbo huku uchunguzi ukiendelea.