Mama Ida: Tumwomboleze Baba kwa amani
MAMA Ida Odinga ametoa wito kwa Wakenya kumwomboleza Raila Odinga kwa amani.
Akizungumza Oktoba 17, 2025 Nyayo Stadium, Mama Ida alisema kuwa Bw Odinga alipenda amani kwa hivyo Wakenya wanafaa kumwoboleza kwa amani.
“Nawaomba tumwomboleze Baba kwa amani. Najua mna machungu sana ila naomba tuomboleze kwa amani,” akasema Mama Ida.
Kando na hayo, aliomba kuwa amani iendelee kudumishwa kote nchini wakati huu ambapo nchi inamwomboleza Bw Odinga.
Mama Ida alisema kuwa wamekaa na mumewe kwa zaidi ya miaka 50 na sio rahisi kumuaga.
Bw Odinga, mwenye umri wa miaka 80, aliangua dunia Oktoba 15, 2025 wakati wa matembezi ya asubuhi ndani ya uwanja wa kituo cha tiba ya Ayurveda, na alikimbizwa Hospitali ya Macho ya Sreedhareeyam Ayurvedic na Kituo cha Utafiti huko Koothattukulam, ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia, msemaji wa hospitali hiyo alisema.