Matokeo ya KCSE kutolewa leo
WAZIRI wa Elimu Bw Julius Migosi Ogamba anatangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne ya mwaka 2024.
Bw Ogamba awali aliongoza maafisa wakuu wa wizara ya Elimu na Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) kufahamisha Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi kabla ya kutangaza matokeo hayo.
Mtihani wa KCSE wa 2024 ulifanyika katika vituo 10,755, ukiwa na idadi kubwa ya watahiniwa 965,501 kutoka 903,138 mwaka wa 2023.
Kutolewa kwa matokeo ya KCSE kunajiri siku moja baada ya Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya kutoa matokeo ya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) 2024.
KPSEA ilifanywa kati ya Oktoba 28 na Novemba 1, huku jumla ya wanafunzi 1,303,913 wa Gredi ya 6 kote nchini Kenya wakifanya mtihani huo
Watahiniwa 1,303,913 waliofanya mtihani wa KPSEA katika vituo 35,573 kote nchini wamejiunga na Gred 7, ambayo bado liko katika shule zao za msingi.