Habari

Mbunge wa zamani Dalmas Otieno afariki akiwa na umri wa miaka 80

Na CHARLES WASONGA September 7th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

ALIYEKUWA mbunge wa Rongo Dalmas Otieno Anyango ameaga dunia.

Kulingana na taarifa kutoka familia yake, Bw Otieno, 80, alikufa nyumbani kwake katika mtaa wa Karen, Nairobi, baada ya kuugua.

Habari za kifo chake zimethibitishwa na mwanawe wa kiume, Eddy Otieno.

Anasema babake alikufa Jumapili asubuhi, Septemba 7, 2025 “kutokana na hitilafu zinazohusiana na shinikizo la damu.”

Mwanasiasa huyo alichaguliwa kwa mara ya kuwa mbunge mnamo 1988.

Baada ya kushinda kiti hicho cha Rongo, Hayati Rais Daniel Moi alimteua Otieno kuwa Waziri wa Ustawi wa Kiviwanda, wadhifa alioushikilia hadi 1991.

Baadaye mwanasiasa huyo alihamishwa hadi Wizara ya Leba ambako alihudumu kwa miaka mitano; kuanzia 1991 hadi 1996, akihudumu kwa muhula wa pili kama Mbunge wa Rongo.

Katika uchaguzi mkuu wa 1997, Bw Otieno alishindwa kutetea kiti chake na akashindwa na Gavana wa sasa wa Migori Ochillo Ayacko.

Bw Otieno pia amewahi kuhudumu kama mwanachama na Naibu mwenyekiti wa Tume ya Kukadiria Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma (SRC)…