Habari

Mfumo mpya wa Safaricom kusaidia kuzima wizi

May 17th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya mawasiliano ya simu Safaricom, imenunua mfumo wa kiteknolojia kutoka Marekani kwa lengo la kusaidia kukabiliana na wizi.

Kampuni hiyo ilinunua mtambo huo kutoka St Loius, kwa kampuni imayofahamika kama Amdocs.

Lengo kuu la kampuni hiyo ni kuimarisha mapato yake katika majukwaa yake yote na kuambatana na mabadiliko ya kiteknolojia, alisema mkurugenzi wa kudhibiti hali hatari Safaricom Nicholas Mulila.

Mwaka 2017, Safaricom ilifuta kazi wafanyikazi 52 walioshukiwa kuhusika katika wizi wa fedha.

Mwaka wa 2016, kampuni hiyo ilifuta 36 walioshukiwa kuhusika katika uhalifu huo.

Kulingana na Bw Mulila, mfumo huo ni dhabiti na utachunga mapato yake katika wakati huu ambapo mambo yamekuwa ya ‘kidijitali’.

Mfumo huo una uwezo wa kuchunguza, kusahihisha, kuzuia pamoja na kuokoa pesa na gharama ya kupotea kwa fedha.

Baadhi ya wafanyikazi walioachishwa kazi ni waliohusika katika kupotea kwa fedha, wizi na ufisadi.