Mkuu wa Keroche akamatwa kuhojiwa DCI
Na MWANDISHI WETU
WAPELELEZI wamekamata Afisa Mkuu Mktendaji wa Keroche Breweries, Tabitha Karanja na watu wengine baada ya kampuni yake ambayo ni maarufu kwa utengenezaji pombe na mvinyo kudaiwa kukwepa ushuru wa Sh14 bilioni.
Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kuagiza Jumatano kukamatwa kwa wamiliki wa kampuni hiyo ambao ni Tabitha na mumewe Joseph Karanja miongoni mwa watu wengine kuhusiana na ukwepaji ushuru.
Waliokamatwa wamefikishwa katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) jijini Nairobi ambapo wanahojiwa.
Tunaandaa habari kamili…