Mwanachuo ashtakiwa kudukua akaunti za benki na kujitumia Sh11.4 milioni
MWANAFUNZI wa chuo kikuu Seth Mwabe Okwanyo amefikishwa kortini kwa kudukua akaunti za benki za kampuni na kujipatia kwa njia isiyo halali Sh11.4 milioni.
Okwanyo alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi Septemba 1, 2025.
Maafisa wa polisi wa kitengo cha Benki Kuu ya Kenya (CBK) waliomba mahakama imzuilie Okwanyo kwa siku 21 kuwawezesha kukamilisha uchunguzi.
Mahakama ilielezwa polisi wanahitaji muda wa kukamilisha uchunguzi na kurekodi ushahidi kabla ya uamuzi kutolewa ikiwa mshtakiwa atafunguliwa mashtaka au la.
Okwanyo aliagizwa azuiliwe hadi Jumatano Septemba 3, 2025 ndipo korti iamue ikiwa itamwachilia kwa dhamana au la.