Habari

Ni kung’aa: Idadi ya waliozoa ‘A’ KCSE yaongezeka kuliko mwaka jana

Na MERCY SIMIYU January 10th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

IDADI ya watahiniwa waliopata alama ‘A’ katika mtihani wa Kidato cha Nne Kenya (KCSE) mwaka 2025 imeongezeka, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu Januari 9, 2026.

Ongezeko hilo linaashiria mwelekeo chanya licha ya changamoto zinazokumba sekta ya elimu nchini.Kwa mujibu wa matokeo rasmi, jumla ya watahiniwa 1,932 walipata ‘A’ mwaka 2025, sawa na asilimia 0.19 ya watahiniwa wote 993,226 waliofanya mtihani huo.

Hii ni ongezeko ikilinganishwa na 2024 ambapo watahiniwa 1,693 pekee, sawa na asilimia 0.18, walipata alama hiyo ya juu zaidi.

Wizara ya Elimu inasema mabadiliko ya mfumo , ufuatiliaji mkali wa mitihani na kuimarika kwa mazingira shuleni ni miongoni mwa sababu zilizochangia hali hiyo.

Shule za kitaifa ziliendelea kutawala katika kutoa wanafunzi waliopata A.

Wakati huohuo, idadi ya wanafunzi waliopata alama za kujiunga moja kwa moja na vyuo vikuu pia imeongezeka.

Jumla ya watahiniwa 270,715 walipata C+ na zaidi.