Habari

Orwoba atimuliwa UDA kwa kuhudhuria hafla ya Matiang’i

Na MWANDISHI WETU May 19th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KAMATI ya Nidhamu ya chama cha UDA imemtimua chamani Seneta Maalum Gloria Orwoba kwa kuhudhuria hafla ya aliyekuwa waziri wa Usalama Fred Matiang’i ya kukutana na wafuasi.

Katika kesi iliyowasilishwa mbele ya kamati hiyo na wanachama Festus Omwamba na Henry Muriithi, wanalalamika kwamba seneta huyo alikiuka sheria ya chama kwa kuhudhuria na kuonekana kujihusisha na chama pinzani.

Inatarajiwa kwamba Bi Orwoba ataenda kortini kupinga kutimuliwa kwake, kama ilivyofanyika wakati wa Millicent Omanga, ambapo alishtakiwa kwa kujihusisha na UDA akiwa angali mwanachama wa Jubilee.