Habari

Pasta Mkenya afurushwa nchini Canada licha ya kusema alitoroka mateso nyumbani

Na HILLARY KIMUYU August 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

JAJI wa Canada ameidhinisha kufurushwa nchini humo kwa mhubiri Mkenya na binti zake wawili baada ya ombi lake kukataliwa.

Rosalind Wanyeki almaarufu Reverend Hadassah, na watoto wake walipangiwa kurejeshwa kutoka jiji kuu la Toronto Alhamisi kupitia ndege ya shirika la Ethiopian Airlines na kuwasili Nairobi Ijumaa adhuhuri.

Bi Wanyeki aliomba muda zaidi Canada, akisema maisha yake yatakuwa hatarini Kenya na kuwa alinuia kuwasilisha maombi ya makao ya kudumu.

Hata hivyo, jaji wa uhamiaji jana aliidhinisha kibali cha kumfurusha baada ya ombi la mwisho la familia hiyo kuhusu hifadhi kukataliwa.

Amedai alitoroka mateso Kenya 2020 na kuhamia Toronto, ambapo anaendesha huduma ya injili.