Habari

Ruto, wandani wake wasikitika baadhi ya mapendekezo ya BBI yanaongeza mzigo

December 2nd, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MWANDISHI WETU

NAIBU Rais William Ruto ameongoza wanasiasa wa mrengo wake katika kikao ambacho wamesema wanataka mpango wa Maridhiano (BBI) uwe wa kuhusisha kila Mkenya na kwamba mapendekezo ya kuongeza viti vya kisiasa yaondolewe kwenye mswada wa marekebisho ya Katiba kupitia kura ya maamuzi.

“Hapa kuna magavana kadhaa, maseneta kadhaa na wabunge zaidi ya 120,” amesema Dkt Ruto akihutubu Jumatano mtaani Karen, Nairobi.

Kiongozi huyo ametaka maswala ya makundi fulani kusalia nyuma kimaendeleo na kuongeza viti ngazi za juu za uongozi, yataongeza mzigo kwa Wakenya.

“Wakati huu tuna Katiba ya 2010 hivyo inawezekana Wakenya wakapigia kura kila pendekezo la kuboresha baadhi ya vifungu katika Katiba,” amesema.

Baadhi tu ya viongozi waliohudhuria kikao hicho na wakahutubu ni Gavana wa Turkana Josphat Nanok, Seneta wa Nakuru Susan Kihika, Seneta wa Meru Mithika Linturi, Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale, Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa miongoni mwa wengine.