Habari

‘Sultan huyo’! Mbunge afichua sababu za viongozi Pwani kumuunga Joho

Na WINNIE ATIENO January 24th, 2026 Kusoma ni dakika: 2

MBUNGE wa Malindi, Bi Amina Mnyazi ameelezea sababu za viongozi wa Pwani kumuunga mkono Waziri wa Madini Hassan Joho, ikilinganishwa na viongozi wengine wa kutoka eneo hilo.

Akizungumza mjini Malindi, Bi Mnyazi alisema viongozi wa Pwani waliamua kumuunga Bw Joho kwa sababu ya uwezo wake wa kuwaunganisha na serikali kuu, kando na kuwasaidia wanapokwama.

Bi Mnyazi alifichua kuwa kulikuwa na shinikizo la kisiasa viongozi wa Pwani wote wahamie chama cha Pamoja African Alliance, inayohusishwa na Spika wa Bunge la Seneti Bw Amason Kingi, lakini walikataa na badala yake kuamua kumpigia debe Bw Joho.

“Tutakwendaje PAA? Hata kama tunataka chama cha nyumbani hatuna kiongozi hapo. Tunampenda Bw Joho na anatusikiza ndio maana tuko naye. Yeye ndiye kiongozi wetu. Kama kweli walikuwa wanataka twende PAA mbona hawajatuita kwenye mkutano na viongozi wote wa Pwani?” aliuliza Bi Mnyazi.

Kufuatia mgogoro katika chama cha ODM, Bi Mnyazi alisema viongozi wa Pwani wameamua kumuunga mkono Bw Joho.

Bi Mnyazi alisema juzi viongozi wa Pwani chini ya vuguvugu la Wabunge wa Pwani (CPG), walikutana na Waziri wa Usalama wa Ndani, Bw Kipchumba Murkomen kuhusu swala la utovu wa usalama eneo hilo.

“Nimekuwa na matatizo ya kiusalama hapa Malindi, nilimtafuta Waziri Murkomen kwa miezi mitano na sikumpata. Nikaenda kwa Bw Joho na akatuandalia mkutano naye na akafanya kikao na wabunge wote wa Pwani,” alisema Bi Mnyazi.

Baadaye, alisema Waziri Joho aliwapangia mkutano wa faragha na Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Kusimamia Bandari Nchini(KPA) kujadili kuhusu miradi ya maendeleo.

Bi Mnyazi alisema wabunge hao walimshinikiza Mkurugenzi Mkuu wa KPA Kapteni William Ruto kuwekeza eneo la Pwani kutokana na mapato ya bandari hiyo ambayo alisema ni raslimali ya wapwani.

“Tulizungumza kuhusu miradi ambayo tunataka KPA itufanyie huku Pwani. Tulitaka kujua miradi ambayo KPA imetekeleza eneo hili. Bandari ni yetu kwanini isiwekeze kwenye miradi ya maendeleo eneo hili? Tulipelekwa na Bw Joho na sasa kuna miradi tutafaidika nayo. Mtu kama Bw Joho nitamuacha kweli?” aliuliza.

Watatu hao walikamatwa mwishoni mwa mwaka jana na wamekuwa kizuizini kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Katika hati za mahakama, mpelelezi mkuu Oliver Nabwone alieleza maendeleo ya uchunguzi, akisema kuwa serikali iko katika hatua za mwisho za uchunguzi kuhusu vifo vilivyotokea Kwa Bi Nzaro.

Nabwone alisema kuwa katika siku 171 zilizotolewa awali kwa uchunguzi, serikali imepiga hatua kubwa na sasa inakamilisha uchunguzi huo.

Alisema kuwa katika siku 60 zilizopita pekee, wachunguzi waliwafuatilia na kurekodi taarifa za familia kutoka kaunti za Migori, Siaya, Homa Bay, Nairobi na Busia ambao jamaa zao wanasemekana kutoweka na wanaaminika kusafiri hadi Kwa Bi Nzaro kwa ibada ya kufunga hadi kufa.

Wachunguzi pia walifanya gwaride zaidi za kutambua washukiwa, wakatathmini eneo la tukio kwa msaada wa Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), na kuwakamata washukiwa zaidi ambao sasa wako kizuizini.

Alisema ushahidi uliokusanywa dhidi ya Anido, Garama, James na Mukonwe ni mzito, na wachunguzi wamependekeza kwa DPP washtakiwe kwa makosa ya mauaji, kueneza misimamo mikali, kuua bila kukusudia na kushiriki katika uhalifu wa kupangwa.

Uchunguzi umebaini kuwa vifo vya Kwa Bi Nzaro havikuwa tukio la pekee bali ni kuendeleza shughuli za dhehebu la Shakahola linalohusishwa na waumini waliosalia wa kanisa haramu la Good News International (GNI) lililoongozwa na Mackenzie.