Thailand kutumia bangi kutibu kansa
NA MASHIRIKA
BANGKOK, Thailand
WIZARA ya Afya Jumatatno ilipokea shehena ya kwanza ya mafuta ya bangi yatakayotumiwa katika matibabu ya kansa.
Waziri wa Afya Anutin Chanvirakul aliongoza hafla ya kupokea chupa 4,500 za mafuta yaliyokamliwa kutoka kwa bangi na Taasisi ya Matibabu ya nchi hiyo.
Waziri alisema kuwa wizara yake inatarajiwa kupata chupa 2,000 zaidi.
Anutin alisema kuwa hospitali zote zitapata dawa ya bangi ya kutosha ndani ya miezi mitano ijayo.
Bunge la Thailand liliidhinisha matumizi ya bangi katika matibabu mwaka jana.
Kulingana na waziri, mafuta hayo ya bangi yanatibu kifaa na kupunguza maumivu haswa wakati wagonjwa wa kansa wanapitishwa kwenye mashine zinazopunguza makali ya saratani, maarufu chemotherapy.
Taasisi ya matibabu iliyokamua mafuta hayo, inasema bangi hiyo imeondolewa kemikali ambazo hulewesha watu. Mafuta hayo pia yatatumika kutibu kifafa.