Habari

Uhuru azuru kaburi la Raila ‘kumtembelea’ siku moja baada ya mazishi

Na MWANDISHI WETU October 20th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta Jumatatu, Oktoba 20, 2025 alizuru kaburi la hayati Raila Odinga, siku moja baada ya mazishi yaliyofanyika Jumapili.

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta katika kaburi la Raila. Picha|Alex Odhiambo

Bw Kenyatta, ambaye siku iliyotangulia alikuwa kwenye hafla ya mazishi ya kitaifa iliyoongwa na Rais William Ruto alifika Kang’o Ka Jaramogi katika kijiji cha Nyamira, Bondo akiwa ameandamana na watu wachache.

Uhuru alipata fursa ya kuamkuana na waombolezaji wengine waliokuwemo mle siku moja baada ya mazishi. Picha|Alex Odhiambo

Alionekana akiweka shada la maua na kutoa sala kabla ya kuanza kusalimiana na waombolezaji wengine ambao bado wamo kwenye eneo hilo.

Uhuru awali, punde habari za kifo cha Raila zilipochipuka alisema ni pigo kubwa la kibinafsi, akisema kwamba Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa rafiki na kakake mkubwa.

“Moyo waniuma sana na kifo hiki, Raila alikuwa kakangu na rafiki yangu ya dhati,” aliandika kwenye ujumbe wa rambirambi.