Habari

Vituo vya karantini vimejaa – Kagwe

June 4th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA ANGELA OKETCH

SERIKALI imeanza mchakato wa kuunda mwongozo wa kuwatunzia nyumbani wanaougua Covid-19 na waliotangamana nao, huku vituo vya karantini vikiendelea kujaa.

Waziri wa Afya Mutai Kagwe Alhamisi alisema kuwa serikali inalenga  kutumia hatua hiyo kupunguza msongamano katika hospitali na vituo vya karantini.

“Kituo cha hospitali ya Mbagathi na kile cha Chuo Kikuu cha Kenyatta vimeanza kujaa wagonjwa wa corona. Wetu wengi walioambukizwa maradhi hayohawaonyeshi dalili zozote na hivyo wanaweza kutunziwa nyumbani,” alisema Bw Kagwe.

Alitangaza hayo huku visa 124 vikiripotiwa Alhamisi na kuongeza idadi kamili ya walioambukizwa kufika 2,340. Kaunti ya Elgeyo Marakwet ndiyo ya hivi majuzi kurekodi kisa cha corona.