Habari

Wakuu wa Keroche waachiliwa kwa dhamana

August 23rd, 2019 1 min read

Na MWANDISHI WETU

WAKURUGENZI wa Keroche Breweries Limited, Afisa Mkuu Mtendaji Tabitha Karanja na mumewe ambaye ndiye mwenyekiti Joseph Karanja wamekanusha mashtaka 10 kuhusu ukwepaji wa ushuru wa Sh14.4 bilioni.

Wakuu hao wa kiwanda cha kutengeneza pombe na mvinyo mjini Naivasha walikamatwa Alhamisi.

Wamefikishwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama jijini Nairobi Bw Francis Andayi.

Tabitha ameachiliwa kwa dhamana ya Sh15 milioni huku Joseph akiachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni pesa taslimu mtawalia.

Aidha, mahakama imeagiza Keroche ilipe Sh15 milioni katika kipindi cha siku saba la sivyo wakurugenzi watakamatwa isipokuwa Afisa Mkuu Mtendaji ambaye ni Tabitha.