Watatu wafariki Viwandani baada ya ukuta kuporomoka
Na SAMMY KIMATU
WATU watatu walifariki Alhamisi huku wengine saba wakipata majeraha na kupelekwa hospitalini baada ya ukuta kuporomoka katika Viwanda vya GilOil vilivyoko kando ya barabara ya Likoni, Viwandani, Nairobi.
Shida ilianza wakati wafanyakazi katika kampuni hiyo walikuwa wakibomoa sehemu moja kwa upanuzi.
Polisi walisema ukuta ulianguka baada ya kuwa dhaifu sana na mawe ya jengo yaliporomoka juu ya miundo kwenye mteremko wa karibu wa mtaa wa mabanda wa Mukuru-Reli.
Ni maiti mbili zilizotambuliwa. Ya kwanza ni ile ya Mellisah Akolo Okwemba ambaye alikuwa mjamzito na akipumzika kwa kitanda ambaye – kulingana na ripoti za wataalamu – alikufa papo hapo.
Mwili mwingine wa Bw James Otieno Nyangasi pia ulikusanywa.
Mtu wa tatu ambaye jina lake halikutolewa alikufa wakati akipelekwa hospitalini.
Mkuu wa Jinai Divisheni ya Makadara, Bw Henry Kiambati ambaye alikuwa katika eneo la tukio alisema kuwa watu wengine saba walipelekwa katika hospitali ya Coptic kando ya Barabara ya Ngong.
Watoto watatu waliwahiwa hospitalini lakini baadaye walikatwakatwa huku watu wazima wanne wakionyeshwa alama za majeraha.
Jamaa wa Familia kwa mmoja wa marehemu alilia kwenye shina hilo lakini alitulizwa na wahudumu wa Msalaba Mwekundu.
Waokoaji walikuwa na wakati mgumu kwa ukosefu wa vifaa na kwa wakati mmoja kamba zilizofungwa kwa tinga ambazo zilifanikiwa kuchukua sehemu katika shughuli za uokoaji zilithibitishwa kuwa bure.
Mhasiriwa, Bi Mary Muthoni mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akiishi katika mtaa wa Mukuru-Reli alishtuka sana alipopata nyumba yake ikiwa imeharibiwa.
“Asante Mungu, hakuna mtu yeyote aliyekuwa ndani ya nyumba wakati tukio hili lilifanyika,” alisema.
Nyumba zilizoathirika ziko kati ya viwanda na nafasi pekee iliyoachwa kati hutumiwa na wapita njia wanaofikia Viwandani na wakaazi wa Mukuru-Reli.
Miezi miwili iliyopita, katika kiwanja cha kampuni hiyo hiyo, nusura wakaazi walioko nyuma ya ukuta wa kampuni hiyo wauawe baada ya korongo kukandamiza paa kadhaa za nyumba. Mwanamke aliponea kifo kwa tundu la sindano.