Habari

Watu kumi wafariki katika ajali ya barabarani

Na MERCY KOSKEI January 5th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

WATU 10 wamethibitishwa kufa baada ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumatatu katika eneo la Karai, kwenye barabara kuu ya Nairobi–Nakuru karibu na mji wa Naivasha.

Polisi na wahudumu wa dharura walisema ajali ilitokea karibu saa tano usiku, wakati basi la abiria lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Magharibi ilipogongana na matatu.

Kwa mujibu wa maafisa, watu wanane waliangamia papo hapo, wakijumuisha abiria wa matatu.

Idadi ya waliofariki iliongezeka hadi 10 baada ya majeruhi wawili kufariki wakitibiwa katika Hospitali ya Kaunti ya Naivasha, ambapo takriban watu 35, wakiwemo watoto watano, walihudumiwa.

Maafisa wa polisi walisema uchunguzi unaendelea ili kubaini sababu kamili ya ajali huku ikisemekana basi lilikuwa likijaribu kupita magari wakati wa msongamano.

Ajali hiyo inajiri siku chache baada ya ajali nyingine ya barabarani kuripotiwa katika eneo hilo iliyomuua aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo.