Habari za Kitaifa

Hata tukichapa lami sasa, tunashukuru kuwa mawaziri

Na BENSON MATHEKA July 12th, 2024 2 min read

SOIPAN Tuya, aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Misitu:

“Chochote kinachofungua njia kwa maslahi ya Taifa letu, kwa wakati huu, ni muhimu zaidi. Namshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais kwa  heshima na fursa ya kutumikia nchi yangu katika wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi, na Idara ya Misitu, kwa miezi 21 iliyopita, moyo wangu umejaa shukrani.”

Aisha Jumwa, aliyekuwa waziri wa Utumishi wa Umma  na Jinsia :

“Nashukuru nilipata nafasi ya kuwatumikia watu wa taifa letu kuu. Asante Mheshimiwa Rais na ninakutakia mema.”

Simon Chelugui, aliyekuwa Waziri wa Ushirika na Maendeleo ya MSME: “Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt William Ruto kwa kuniamini na kunikabidhi kazi na wajibu wa kuhudumu katika baraza la juu zaidi la maamuzi la Jamhuri ya Kenya kama waziri.”

Aden Duale, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi:

“Namshukuru rais kwa fursa ambayo alinipa kuwa Waziri wa Kwanza wa Ulinzi chini ya utawala wa Kenya Kwanza.

Kipchumba Murkomen, aliyekuwa waziri wa barabara na uchukuzi:

“Imekuwa fursa yangu kubwa na heshima kutumikia nchi yangu kama waziri anayesimamia Barabara na Uchukuzi. Asante mheshimiwa Rais kwa kunipa nafasi. Mungu akubariki na Mungu ibariki Kenya.”

Susan Nakhumicha, aliyekuwa waziri wa Afya :

“Ninajivunia timu ya Wizara ya Afya ambayo ni mama mzazi wa mageuzi( katika sekta ya afya) washirika wa maendeleo na bunge ambalo lilipitisha miswada wa Afya ya Jamii, “Shukrani kwa wahudumu wa Afya kwa msaada na moyo wangu unawaendea Wahudumu  wa Afya ya Jamii wanaozingatia kauli mbiu yetu “Afya Nyumbani”. aliongeza.

Ababu Namwamba,aliyekuwa Waziri wa Michezo:

“Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa Imani kwangu iliyomfanya  kuniteua waziri kwa mara ya pili katika maisha yangu ya utumishi wa umma.Mungu ibariki Kenya na amjalie Rais neema na hekima kuelekeza nchi yetu.”

Alice Wahome, aliyekuwa waziri wa Ardhi:

Shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt William Samoei Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, kwa nafasi uliyonipa ya kuhudumu kama waziri Ardhi, Ujenzi, Nyumba na Maendeleo ya Miji na hapo awali kama Waziri Maji, Usafi wa Mazingira na Unyunyuzaji. Nitaendelea kukuunga mkonohasa wakati huu ambapo Taifa letu linahitaji mikono na nguvu zote kuliunganisha pamoja ili kujenga kenya yenye nguvu na thabiti.