AFYA: Umuhimu wa ulaji wa maharagwe
Na MARGARET MAINA na MAJARIDA YA AFYA
MAHARAGWE kwa kawaida ni mbegu za jamii ya kunde lakini kubwa na hupikwa kama chakula au kitoweo. Ni chakula ambacho baadhi ya watu hukichukulia kama chakula cha hadhi ya chini kisichokuwa na manufaa kiafya.
Hata hivyo, maharagwe yana faida nyingi sana mwilini ambazo watu wasiokula maharage kama yanavyojulikana pia, huzikosa.
Maharagwe hupunguza lehemu (cholesterol)
Moja kati ya vyakula vinavyopunguza lehemu mwilini ni maharagwe. Nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye maharagwe hujishikiza na lehemu ziwapo tumboni na kuzuia lehemu zaidi kufyonzwa na kuingia mwilini ovyo.
Huboresha afya ya ubongo
Thiamine pamoja na Vitamini K zinazopatikana kwenye maharagwe husaidia katika kuboresha afya ya ubongo.
Husaidia katika kudhibiti kiwango cha sukari mwilini
Kwa kiasi fulani, maharagwe yana nyuzinyuzi ambazo hupunguza kiwango cha metaboli ya wanga (carbohydrates) mwilini. Kwa kufanya hivi, huwezesha kutawala kuongezeka kwa kiwango cha sukari hasa baada ya kula chakula.
Maharagwe pia yana protini ambayo husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Huongeza nguvu za mwili
Kuwepo kwa madini ya chuma pamoja na manganese kwenye maharagwe kunayafanya kuwa na nafasi kubwa katika kuongeza nguvu za mwili.
Madini haya ni muhimu sana katika kuuongezea na kuupa mwili nguvu.
Huimarisha mifupa
Madini ya calcium pamoja na manganese ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya mifupa. Maharagwe ni chanzo kizuri cha madini haya.
Huboresha ngozi
Maharagwe husaidia michakato ya metaboli ya asidi ya amino, gluconeogenesis, neurotransmitter synthesis, histamine synthesis, asidi ya mafuta (fatty acids), lipids and hemoglobin synthesis kwenda vizuri.
Huboresha afya ya macho
Madini ya zinc yanayopatikana kwenye maharagwe ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya macho. Hivyo basi ulaji wa maharagwe mara kwa mara utaboresha afya ya macho yako.
Huboresha uwezo wa kumbukumbu
Vitamini B1 inayopatikana kwenye aina mbalimbali za maharagwe hukabili ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer’s na Dementia).
Huboresha afya ya kucha na nywele
Biotin, madini ya chuma pamoja na protini; vyote vikipatikana kwenye maharagwe, vina nafasi kubwa katika kukupa kucha imara pamoja na nywele zenye afya njema.