AFYA: Faida za majani ya giligilani/ korianda katika mwili wa binadamu
Na MARGARET MAINA
WENGI wetu tunayatumia majani haya katika mapishi mbalimbali kuongeza ladha kwenye vyakula, lakini pia majani haya yana manufaa muhimu katika miili zetu kama vile:
Kusaidia mmeng’enyo wa chakula
Mbegu za korianda na majani yake zinasaidia kwenye utendaji kazi wa ini na pia kuufanya mwili uzalishe vimeng’enyo vinayotumika katika kusaga chakula.
Kutibu vidonda vya tumbo
Korianda ni chanzo kizuri cha Folic acid, Vitamini C, Vitamini A na Beta carotene. Mbegu za korianda na majani yake huwa na asilimia 30 ya Vitamini C.
Hii inasaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali pia kusaidia kuponyesha vidonda. Uwepo wa kiwango kikubwa cha Vitamini C hukupa uhakika wa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo, mafua na midomo kuchibuka.
Kinga ya kisukari
Matumizi ya korianda yanahusishwa zaidi na kupungua kwa maradhi ya kisukari mwilini. Hii ni kutokana na kuwa korianda huchochea uzalishaji wa insulin ambayo hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
Vilevile, korianda hupunguza kiwango cha lehemu mbaya na kuboresha kiwango cha lehemu nzuri kwenye damu. Watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na wale wenye lehemu nyingi mbaya wanashauriwa kunywa maji ya korianda kila siku ili kupunguza maradhi haya.
Kukinga Anaemia
Korianda zina kiwango kikubwa cha madini ya chuma yanayosaidia kuongeza kiwango cha damu.Ni vizuri kutumia korianda na majani yake kwenye milo yetu ya kila siku.
Kutoa uchafu na sumu mwilini (Detoxification)
Kuna baadhi ya vyakula vina mkusanyiko wa kiwango kidogo za chembechembe zenye sumu. Ulaji wa hivi vyakula hulimbikiza hizi sumu kwenye damu na huweza kuleta magonjwa ambao humfanya mgonjwa apoteze kumbukumbu na mishipa ya damu kushindwa kufanya kazi. Korianda husaidia kufyonza sumu zilizomo kwenye damu na kuzitoa bila kuleta madhara mwilini.
Kuzuia magonjwa ya macho
Korianda ni moja ya tiba conjunctivitis kwa kupunguza wekundu, kuwasha na kuvimba macho.
Kutibu chunusi
Korianda hutumika kutibu chunusi na madoadoa kwenye ngozi. Changanya korianda, asali na manjano kisha paka kwenye sehemu zilizoathirika.
Kama ngozi ni kavu, safisha kwa maji baridi kabla ya kupaka.
Kuboresha afya ya nywele
Changanya korianda ya unga pamoja na mafuta ya nywele kisha paka kwenye ngozi mara mbili kwa wiki.
Hii inasaidia nywele ziache kukatika na kuzifanya imara na zenye afya kuanzia kwenye mizizi.