Makala

AFYA: Jinsi ya kula mlo unaofaa

May 16th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KUANZA kula mlo kamili na bora kunaweza kuwa ni kazi pia kwa sababu baadhi ya watu hushindwa kutokana na sababu kadhaa.

Katika baadhi ya familia kumejengeka mazoea kiasi kwamba “tukiamka asubuhi ni viporo, vitumbua na kadhalika, mchana ni ugali na usiku ni wali.

Hizi hapa ni baadhi tu ya njia za kukusaidia kula mlo kamili:

Anza kwa kuhesabu matokeo

Jiulize maswali kama vile: “Ni nini unapata kutokana na mlo unaokula sasa?”

Wengi tunaichukia miili yetu kwa kuwa minene au kutokeza vitambi na kuchukia baadhi ya maeneo mengine ya miili yetu. Lakini hayo si matokeo ya pekee ambayo tunaweza kusema ni hasi kwa sababu kuna yale hatari kama:

  • matatizo ya moyo
  • hatari ya kupata saratani
  • kunenepa kupita kiasi
  • kuanza kujichukia

Baadhi ya faida za kula mlo kamili na bora ni zifuatazo:

  • hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa
  • hufanya mtu awe mwenye kujiamini
  • huupa mwili nguvu

 

Hivyo unashauriwa ujifunze faida za vyakula mbalimbali kwa sababu kwa sababu kufanya hivi kutakusaidia kujua kipi kinakufaa na kipi hakikufai.

  • jielimishe kuhusu vyakula bora
  • anzisha urafiki na watu wenye lengo moja na wewe
  • jifunze kupika vyakula bora na vya kisasa ili uweze kufurahia mlo wako

Anza taratibu

Kosa kubwa ambalo watu wengi hulifanya ni kutaka kuanza kwa ukubwa.

anza kwa kupunguza milo fulani taratibu kama kupunguza unywaji chai na sukari nyingi, kupunguza kula viporo au vitumbua.

  • kunywa green tea badala ya kahawa
  • kunywa maji na juisi ya matunda badala ya soda
  • kula wali wa kahawia badala ya wali mweupe
  • mafuta ya nazi au mizeituni badala ya yale processed ya kupikia

Jifunze upishi rahisi wenye ambao huhitaji muda mchache 

Jifunze mapishi rahisi ya mlo kamili; hii itakusaidia kuepukana na kununua vitu vya madukani au junk food; fanya hii iwe tabia yako.

Unaweza kutafuta siku mbili au tatu ukapika vyakula vingi na kuvihifadhi kwenye jokovu ili pale usikiapo njaa unapasha moto na kula badala ya kwenda kununua chipsi au burger.

Rembesha sahani yako 

Vyakula hivi vinaweza visiwe na sura nzuri sana usoni mwako na ndiyo maana ni jambo jema kujaribu kuvifanya viwe vizuri kadri ya uwezo wako.

Ili kuleta hamu ya kuvila, ongeza ladha unazozipenda, weka vitu vya rangi rangi kama karoti, pilipili mboga za kijani, manjano, nyekundu na kadhalika.