Makala

AFYA: Manufaa ya mbegu za chia katika mwili wa binadamu

February 27th, 2020 Kusoma ni dakika: 2

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MBEGU za chia ni mojawapo ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha virutubisho.

Zina virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa afya ya mwili na ubongo.

Virutubisho vilivyo ndani ya mbegu za chia ni:

  • Omega- 3
  • vitamini
  • protini
  • Nyuzinyuzi (fibre)
  • Mafuta ya Omega 3, na Omega 6
  • Calcium
  • Manganese
  • Magnesium
  • Phosphorous

Pia mbegu hizi zina Vitamini A, B, D na E, na kemikali za kulinda mwili (anti-oxidants)

Faida za chia kiafya

Kulainisha ngozi na kupunguza dalili za uzee

Ndani ya mbegu hizi kuna kemikali zinazosaidia kupunguza makali ya radikali huru (free radicals) zinazotengenezwa katika miili yetu na kuleta matatizo mbalimbali kwenye ngozi.

Anti-oxidants zinasaidia kutengeneza seli mpya za ngozi na kuondoa zile zilizokufa hivyo kuzuia ngozi kuharibika na kuwa na makunyanzi,Pia kutumia mbegu hizi inasadia kuepusha seli za ngozi kufa kabla ya muda wake kutokana na magonjwa.

Mfumo wa kumeng’enya chakula

Mbegu za chia zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi. Nyuzi hizi zinasaidia sana katika kumeng’enya chakula.

Mbegu hizi zinasaidia kupunguza uzani kwa watu wenye uzani uliopitiliza.

Afya ya moyo

Mbegu za chia zinasaidia mwili katika kiwango cha Lehemu na kupunguza hatari ya mtu kupata tatizo la mishipa ya damu kujaa mafuta. Hivyo, mbegu hizi ni muhimu katika kuimarisha afya ya moyo na kuondoa hatari ya kupata tatizo la shinikizo la damu kuwa juu.

Afya ya ubongo

Chia seeds zina kiwango kikubwa cha Omega -3 na Omega- 6 Fatty acids ambazo ni muhimu sana katika kusaidia ubongo kutengeneza seli zake. Virutubisho hivi ni muhimu sana kwa watoto.

Kuupa mwili nguvu

Matumizi ya mbegu za chia huupa nguvu mwili mara mbili ya jinsi vinywaji vya kuongeza nguvu kama lucozade vinavyoweza kuongeza nguvu ya mwili.

Kuimarisha mifupa

Kama tulivyoona mbegu hizi ndani yake kuna kiwango kukubwa cha madini ya calcium hivyo husaidia kuimarisha mifupa,

Afya ya meno

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya calcium, phosphorous, vitamin A na zinc, mbegu hizi zinasaidia kuimarisha afya ya meno pia.