• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
DKT FLO: Ninapatwa na matatizo ya UTI kila tunapojamiiana na mume wangu!

DKT FLO: Ninapatwa na matatizo ya UTI kila tunapojamiiana na mume wangu!

Mpendwa Daktari,

MUME wangu anafanya kazi katika mji wa mbali ambapo sisi hukutana kati ya miezi miwili na mitatu. Tatizo ni kwamba nimekuwa nikikumbwa na matatizo ya Urinary Tract Infection (UTI) kila baada ya kushiriki tendo la ndoa naye.

Je, maambukizi haya ni maradhi ya zinaa? Na je, anaweza kuwa na uhusiano wa pembeni au kuna jambo jingine linalonisababishia maambukizi haya?

Christine, Nairobi

Mpendwa Christine,

UTI ni maambukizi yanayoukumba mfumo wa mkojo, kutoka kwa figo hadi kwa urethra.

Kwa hivyo, la, si maradhi ya zinaa. Kwa wanawake, maradhi ya zinaa huathiri mfumo wa uzazi na mara nyingi husababisha uowevu wenye harufu mbaya kutoka ukeni, sehemu ya uke huwasha, hupata uchungu wakati wa tendo la ndoa na maumivu sehemu ya chini ya tumbo.

Pia yaweza sambaa na kuufikia mfumo wa mkojo na kusababisha maumivu wakati wa kuenda haja ndogo, kuhisi haja kila mara na maumivu sehemu ya chini ya tumbo.

Yawezekana kwamba maambukizi ya kila mara ya UTI yanasababishwa na honeymoon cystitis; hali inayomkumba mwanamke anaposhiriki tendo la ndoa baada ya kukaa muda mrefu.

Maambukizi ya UTI husababishwa na bakteria ya kawaida kwenye ngozi ya mwenzako unayeshiriki naye tendo la ndoa, ambayo hupitishwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa baada ya kukawia kabla ya kufanya hivyo.

Aidha, maambukizi haya ya kila mara yaweza kutokana na maradhi ya zinaa. Ni muhimu kujua iwapo pia mwenzako anaonyesha ishara hizi na ni vizuri ikiwa mtafanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Pia, unapaswa kufanyiwa uchunguzi wa mkojo na sehemu ya uke kutambua iwapo mfumo wa uzazi umeathiriwa. Nyote mnapaswa kuoga kabla ya kushiriki tendo la ndoa na kuenda haja ndogo pindi baadaye kuhakikisha kwamba mnaondoa aina yoyote ya bakteria ambayo huenda imeingia kupitia urethra.

Vilevile, wakati wa kushiriki tendo la ndoa tumia mafuta ya kulainisha ili kupunguza msuguano. Kunywa maji kwa wingi na uhakikishe kwamba choo ni kisafi kabla ya kukitumia. Aidha, unapojipangusa baada ya kuenda haja kubwa, jipanguse kuanzia mbele ukirudi nyuma.

  • Tags

You can share this post!

Savula na wake zake wawili kuongezewa mashtaka mengine ya...

Nilikula uroda na rafiki ya mzee balaa ikatokea, nishauri

T L