• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Ubora wa mbegu za kiume hushushwa na hewa chafu

Ubora wa mbegu za kiume hushushwa na hewa chafu

NA CECIL ODONGO

Kupumua hewa chafu kunasababisha mwanaume kuwa gumba, watafiti wamebaini.

Watafiti kutoka Uingereza waliafikia hilo mapema mwezi huu baada ya kugundua kuwa hewa chafu huathiri kutengenezwa kwa mbegu za kiume na husababisha mwanaume kukosa kuzalisha.

Kwa mujibu wa watafiti hao mwiingiliano wa hewa chafu na ile safi una madhara hasi kwa mbegu za kiume na pia huchangia tatizo la uume kukosa kupata ashiki kabla ya tendo la ndoa.

Takwimu za kiafya ulimwenguni zinaonyesha kuwa kupumua hewa chafu ni hatari ni kumesababisha vifo vya watu bilioni 2.4 huku kila mwaka maafa 6.5 milioni yakiripotiwa.

Kaboni, nitrojeni, ozoni na Salfa ni hewa chafu ambazo watafiti hao waligundua zinaathiri mbegu za kiume na kushusha ubora shahawa (semen), kando na kuchangia matatizo mengine ya kiafya.

Kati ya matatizo yanayosababishwa na kupumua hewa chafu ni msongo wa mawazo, wasiwasi na pia afya ya kiakili ya mwanaume huathirika.pamoja na pia kuyapata magonjwa ya moyo.

Wakati wa utafiti huo, ilibainika kuwa tafiti nyingi zinazoendelea kufanywa zinaonyesha kuwa wanaume wengi wana mbegu hafifu za kiume na baadhi wameishiwa kuwa gumba (kukosa uwezo wa kuzalisha).

Kwenye uundaji wa mbegu za kiume, hewa chafu ni hatari kwa sababu huua seli ambazo ni muhimu katika mchakato wote huo. Isitoshe, homoni za uzazi huvurugika huku baadhi ya seli nazo zikitanuka na kushusha ubora wa mbegu za kiume zinazotengenezwa.

Japo tafiti nyingi zinaonyesha athari hasi ambayo hewa chafu inayo katika kuundwa kwa mbegu za kiume, bado utafiti zaidi unahitajika kufahamu baadhi ya masuala tata kwa undani.

Kwa upande mwingine, wanasayansi wanapendekeza kuwe na hamasisho kuhusu kuzuia uchafuzi wa mazingira ili kuzuia kupanda kwa wanaume ambao ni gumba kwa kupumua hewa chafu.

  • Tags

You can share this post!

Wanaohusudu tohara ni wapumbavu, Raila asema

Msichana atembea 15km kujiunga na shule akiwa hana hata...

T L