Afya na Jamii

Usihangaike, jaribu vyakula hivi ukiwa unapanga kupunguza uzito

Na PAULINE ONGAJI May 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KUPUNGUZA uzani si jambo rahisi kwa wengi hasa kwa sababu mara nyingi huhusisha kufanya mazoezi.

Kwa hivyo, kuna baadhi ya watu ambao wamelazimika kutumia njia za mkato ili kupunguza uzani, na katika harakati hizo kuhatarisha afya na maisha yao.

Ikiwa wewe ni mmoja wao, haina haja ya kufanya hivyo.

Badala yake, sasa waweza anza kula vyakula vitakavyokusaidia kupunguza huo uzani unaokusumbua. Baadhi ya vyakula vinavyosaidia kupunguza uzani ni pamoja na:

Maji

Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tokyo, unapokula vyakula vilivyo na viwango vya juu vya maji kama vile matunda na mboga unashiba upesi na hivyo kukuepusha usile chakula kingi.

Brokoli

Mboga hizi zina viwango vya juu vya nyuzi na madini ya calcium, viungo muhimu katika ukuzaji wa misuli.

Kabeji

Mboga hii ina kiwango cha juu cha kemikali za kusfisha mwili kama vile vitamin C, mbali na kuimarisha hali ya kinga mwilini.

Koliflawa

Sawa na mboga zingine, koliflawa ina viwango vya juu vya virutubisho vya vitamini C na folate. Inapoliwa ikiwa bichi au ikipikwa kwa muda mfupi basi unaongeza uwezo wake wa kusafisha damu.

Balungi

Tunda hili lina viwango vya juu vya vitamini C, folic acid, na potassium.

Saladi

Kwa kawaida chakula hiki huwa na kiwango cha juu cha B vitamins, folic acid, na manganese, virutubisho muhimu
vinavyodhibiti viwango vya sukari kwenye damu na ni muhimu kusaidia kuimarisha kinga mwilini.

Figili

Mboga hizi zina viwango vya juu vya madini ya potassium, folic acid, sulfur na kemikali za kusafisha mfumo wa mwili na hivyo kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

Spinachi

Mboga hizi zina viwango vya juu vya madini ya chuma, folic acid, na vitamin K. Kadhalika zina viwango vya juu vya kemikali za kupambana na maradhi.

Unapoandaa chakula hiki hakikisha haukipiki kwa muda mrefu.